Wolper afunguka kuhusu ushoga wa Bwana ake
Picha ya mpenzi wake Wolper, Brown ambayo imezua gumzo mitandaoni.
Ili kupata mbivu na mbichi za sakata hilo, Wikienda kama kawaida yake lilimtafuta Wolper na kumuweka ‘mtukati’ ambapo alifunguka kuwa, katika maisha yake amepitia vitu vizito, jambo ambalo linamfanya kuwa na ujasiri wa kukabiliana na mambo kama hayo anayokutana nayo kwa sasa.
Wolper alisema kuwa, mpenzi wake huyo alishampa taarifa kuwepo kwa picha hizo muda mrefu akijua wazi ipo siku watu watazisambaza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kujua yupo naye kimapenzi.
“Katika maisha haya nimekutana na vitu vingi sana, tena vingine ni vigumu mno, kwa hiyo jambo hili kwangu halinipi shida, ni jambo dogo mno na uzuri alishawahi kunieleza,” alisema Wolper.
Staa huyo aliendelea kuweka wazi kwamba, anajua fi ka watu wanafi kiri atamuacha Brown kwa sababu ya skendo hiyo lakini ukweli ni kwamba watakuwa wanajisumbua kwani yeye kwake anaona ni jambo dogo mno.
“Mbona hizo picha hazikusambaa zamani mpaka sasa hivi yupo na mimi ndiyo ionekane ni dili? Mimi sitetereki,” alisema Wolper.
Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anachojua ni kwamba picha hizo zilipigwa wakati jamaa huyo akiwa kwenye kazi yake ya uanamitindo na anajua wazi kuna watu wanaocheza mchezo huo ili wamuumize na kumuharibia bwana’ke huyo.
Wikienda halikuishia hapo kwani lilimtafuta Brown ili kuzungumzia jambo hilo ambapo alisema kuwa, alijua tu ipo siku picha hizo zitasambazwa, lakini hakuona ubaya wowote kwani ni picha ambazo wako kazini.
“Ninajua mengi yatatokea kuhusiana na hizo picha, lakini uzuri nil ishamwambia Wolper, kwa hiyo sioni kama linanisumbua sana,” alisema Brown.
Comments
Post a Comment