CHEMICAL afunguka kuhusu muonekano wake mpya

Rapa wa kike anayefanya vizuri na ngoma ya 'Queen Of Dar es salaam', Chemical ameweka wazi sababu ya kukubali kubadili muonekano kwenye video mpya ya Msami 'So Fine' iliyotoka hivi karibuni ni kutaka kujiona yeye mwenyewe kwenye muonekana mpya. 

Akifanya mahojiano na EATV Website, Chemical amesema baada ya Msami kumuelekeza kwamba anamuhitaji Chemical wa aina gani ilimfanya awe mpole hata wakati wa kufanyiwa 'Make up' ili kipatikane kitu ambacho kilidhamiriwa ingawa siyo mashabiki zake wote waliofurahi kumuona katika muonekano wa aina hiyo. 

"I was so excited like Ok na mimi nataka kujiona nitakuaje kwa hiyo kuanzia make up mpaka mavazi hakuna mahali niliongea niliambiwa vaa hivi nikakubali na kila kitu alikuwa ni Msami.  Kwa hhiyo watu wasiseme kwa Chemical hawezi kuwa hivi au kuvaa hivi nataka tu wajue kwamba naweza kuwa mtu yoyote ambaye nataka kuwa" amesema. 

Pamoja na kuonekana na mabadiliko makubwa katika video hiyo Chemical amedai kuwa hawezi kuwaahidi mashabiki zake kama ataweza kuendelea na muonekano mpya au ule wa zamani kwani yeye ni msani. 

"Chemical ni yuleyule kama kutakua na mabadiko yanahitajika kufanywa yatafanyika lakini muonekano wangu wa awali ulinitambulisha na watu walinikubali vile nilivyokuwa. Nilifanya vile pia kujua  watu wanamtaka chemical wa aina gani ingawa mpaka sasa ni 50/ 50 wapo walionikubali lakini wapo walioponda" ameongeza

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya