MJADALA MZITO simba KUHUSU KUMVUA UKAPTENI mkude

Taarifa za uongozi wa timu ya Simba pamoja na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Joseph Omog kumvua unahodha kiungo wake wa kutumainiwa Jonas Mkude limeendelea kuzua mjadala ambapo nahodha wa zamani wa timu hiyo, Henry Joseph amefunguka.

Henry Joseph maarufu kwa jina la 'Shindika' ameongea na gazeti la Mwananchi kutokea nchini Norway ambapo alisema wazi kuwa timu hiyo imefanya jambo lisilo la kiungwana kulinganisha na kazi yake aliyoifanya ndani ya timu hiyo.

Shindika alisema kiungo huyo hata kama alikuwa na makosa binafsi lakini sio sababu ya yeye kuvuliwa jumla uongozi huo badala yake ilipaswa angalau apewe unahodha msaidizi ambapo alishauzoea.

"Kiukweli mimi sijafurahishwa na uamuzi uliofanywa na timu kumvua unahodha kulingana na kazi kubwa anayoifanya uwanjani lakini pia ingependeza zaidi kama wangemfanya nahodha msaidizi," alisema Shindika.

Katika hatua nyingine Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars mbali na kukumbushia jinsi yeye mwenyewe alivyovuliwa Unahodha wa timu ya taifa bila kuelezwa sababu ikiwa ni pamoja na ilivyokuwa kwa Nadir Haroub Canavaro alihoji kwanini suala hilo linajirudia.

"Hili la Mkude limenigusa kwa kuwa ni suala ambalo lilinikuta hata mimi kwenye timu ya Taifa kuvuliwa unahodha bila kuelezwa lakini pia hata Nadir alifanyiwa hivi kwanini linajirudia?”, alihoji

Shindika hivi sasa yupo Norway ambapo hata hivyo hakuweka wazi ameenda kufanya nini nchini humo zaidi ya kudai yupo mapumzikoni.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).