DONALD NGOMA :Nipo tayari kuwapa RAHA Yanga
- Get link
- X
- Other Apps
Donald Ngoma anatarajia kuanza mazoezi na kikosi cha Yanga, kesnho, baada ya kupona tatizo lake la goti ambalo limemweka nje kwa muda mrefu msimu uliopita.
Ngoma amekiambia chombo kimoja cha habari, kwa njia ya mtandao kuwa kwasasa amepona kabisa tatizo lake la goti na yupo tayari kuanza kuipigania timu yake kwenye msimu ujao wa ligi ya Vodacom itakayoanza Agosti 26 mwaka huu.
“Nipo fiti nimepona kabisa tatizo la goti nilikuwa hapa Afrika Kusini kwa muda nikifanyiwa matibabu lengo ni kutimiza majukumu yangu vizuri nikiwa na Yanga,’amesema Ngoma.
Mshambuliaji huyo amesema anatarajiwa kurejea Dar es Salaam leo Jumapili na Jumatatu atakuwepo kwenye kikosi cha Yanga ambacho kitaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu ujao.
Amesema anataka kuifanyia mambo makubwa timu hiyo katika msimu ujao hivyo mabeki wa timu pinzani wajiandae kwani hatokuwa na msalie mtume.
Amesema anataka kulipa fadhila baada ya msimu uliopita kukaa nje kwa muda mrefu na kushindwa kuipigania timu hiyo ambayo alijiunga nayo misimu miwili iliyopita.
Ngoma hivi karibuni amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga timu ambayo ameitumikia kwa mafanikio makubwa akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe.
By Godfrey Mpagike
@Skeleton boy
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment