YANGA KUJICHIMBIA MOROGORO

Image result for yanga photos
Image result for yanga photos
TIMU ya soka ya Yanga inaingia kambini wiki ijayo Morogoro kujiandaa na Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu ujao.
Tayari wapinzani wao, Simba wako kambini nchini Afrika Kusini kujiandaa na ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 26, 2017. Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe (pichani) alisema wamechagua Morogoro kwani kuna mazingira tulivu yatakayowasaidia.
Alisema wachezaji wote waliosajiliwa wataenda ili kutoa nafasi kwa Kocha kutengeneza kikosi bora cha msimu ujao. Yanga imesajili wachezaji kadhaa na kuwaongezea mkataba waliomaliza.
Imewasajili Ibrahim Ajibu, Youthe Rostand, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ Baruan Yahya, Pius Buswita na imewaongezea mkataba Donald Ngoma, Amis Tambwe na Thaban Kamusoko. Yanga itacheza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Lipuli FC ya Iringa Agosti 27, uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya