MSUVA DEAL DONE morocco
ALIYEKUWA winga machachali wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simon Happygod Msuva ametangazwa rasmi kujiunga na Klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco kuitumikia timu hiyo.
Msuva ambaye ni mfungaji bora wa Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/17 amejiunga na klabu hiyo ikiwa ni siku mbili tangu aondoke Tanzania kwenda nchini humo kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kujiunga nayo.
Msuva amepata nafasi ya kujiunga na Defaa El Jadida kwa mkataba wa miaka mitatu na tutamuona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiichezea El Jadida ambayo imemaliza msimu ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Wydad Casablanca kwa tofauti ya point saba.
Msuva sasa anaungana na Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyekuwa akiichezea Klabu ya Simba na baadaye Azam FC ambaye pia amejiunga na Difaa El Jadida.
Comments
Post a Comment