RIHANNA NI MJAMZITO AU
Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’.
MWANAMUZIKI, Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ anadaiwa kuwa mjamzito kutokana na muonekano wake kifuani, usoni, matendo na mavazi.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja umedai kuwa, Rihanna anadaiwa kushika ujauzito wa mpenzi wake Bilionea Hassan Jameel ambapo ameongezeka uzito wa pound 50 (kilo 23) tofauti na kawaida.
Julai Julai 25, mwaka huu Rihanna alionesha vazi lake jekundu lililoonekana la hadhi kubwa ambalo lilipendwa na wanamitindo alipokuwa kwenye maonesho huko London ndipo maneno ya kuwa mjamzito yalipoanza kuvuma huku watu wakidai kuwa maziwa yake na uso uliojaa ndiyo unaoonesha kuwa ni mjamzito.
Comments
Post a Comment