Yanga yahamia rasmi uwajani


Kikosi cha Yanga jana kilianza mazeozi mepesi ya uwanjani baada ya kuwa kimemalizana na yale ya gym.

Lakini leo, kikosi hicho kitaanza mazoezi makali rasmi ikiwa ndiyo mazoezi ya kwanza makali katika kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2017-18 lakini pia michuano ya Kombe la Shirikisho na michuano ya kimataifa.

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema mazoezi ya jana ilikuwa ni sehemu ya kupasha miili moto.

“Tulikuwa tunatoka katika mazoezi ya gym kuingia uwanjani. Kawaida lazima uangalie mabadiliko ya miili,” alisema.

Yanga ambayo inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya