HAJI MANARA.Kaseke amekimbia swaumu


Muda mfupi baada ya kiungo Deus Kaseke kusajiliwa na Singida United akitokea Yanga, Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametupa dogo kwa wapinzani wao wa jadi Yanga juu ya usajili huo.
Kaseke amesajiliwa Singida baada ya mkataba wake kumalizika kisha kutoafikia katika makubaliano kati yake na Yanga ambapo suala la kimaslahi linadaiwa kuwa ndiyo chanzo cha kutosaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameweka picha ya Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali akiwa anakula, kisha akaandika hivi:
“Mhenga aliyesema mtegemea cha ndugu hufa maskini, kweli yametimia, Kaseke kashindwa kuvumilia swaumu, inaitwa NDI NDI NDI.”
Baada ya kuandika hivyo, Kaseka akawa tag Kaseke mwenyewe, Lady Dee, Mrisho Ngassa na Juma Kaseja.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya