SAFARI YA KICHUYA YATIMIA SASA
Siku chache baada ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika Klabu ya AFC, mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya anaweza akapata shavu la kucheza soka nchini Misri.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema klabu moja ya Misri inamtaka Kichuya ili imsajili kwa ajili ya kuichezea timu yao na sasa wapo katika mazungumzo.
Bado mazungumzo ya Simba na klabu hiyo yanaendelea na wakifikia muafaka muda wowote Kichuya ataondoka kwenda nchini humo.
“Kuna timu ya Misri kupitia wakala aliyemuona Kichuya kwenye ligi na kufanya mawasiliano na sisi na tayari kuna barua wameleta wakimtaka Kichuya.
“Kuna dau ambalo wamelipendekeza ili waweze kumsajili Kichuya lakini sisi hatujakubaliana nalo, hivyo tupo katika mazungumzo ya kuweza kufikia makubaliano lakini tunataka waongeze dau.
“Hata hivyo, itabidi tumuachie Kichuya akacheze soka la kulipwa kwani kumzuia mchezaji kwa sasa ni sawa na bure, kwani amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na hatutaki baadaye aende bure.
“Maongezi yanaonekana kuendelea vizuri na wakati wowote mambo yatakaa sawa kwani klabu yenyewe haimuhitaji mchezaji kwa ajili ya majaribio na badala yake kwenda kucheza moja kwa moja,” alisema bosi huyo.
Comments
Post a Comment