SUGU:Nataka niajiri zaidi ya watu 5000

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Joseph Mbilinyi amesema ndoto yake ni kuja kuajiri watanzania zaidi ya 5000 katika shughuli mbalimbali ambazo atazianzisha siku za usoni. 

Sugu ambaye ni mmiliki wa hotel ya Desderia ambayo inatarajiwa kufunguliwa muda si mrefu jijini Mbeya amesema kwa kuanza kwa mwaka huu ataajiri Watanzania zaidi ya 50 katika hotel hiyo na kudai lengo lake kubwa ni kuja kutoa ajira zaidi kwa watanzania wenzake. 

"Rapa ambaye nimebadilika na kuwa muajiri hivi sasa, kwa mwaka huu nitatoa ajira kwa watanzania wenzangu zaidi ya 50 lakini lengo langu ni kuajiri watu si chini ya 5,000 kwa miaka 10 ijayo kama Mungu ataendelea kunipigania" alisema Jongwe 

Mbali ya kuanzisha hotel hiyo mbunge na msanii huyo alikuwa na mpango wa kutengeneza pombe kali ambazo alikuwa akizitambulisha kwa jina la 'Deiwaka Gin' ambazo zilitakiwa kuanza kutoka chini ya kampuni yake ya Deiwaka.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya