Kisa cha PETER MANYIKA kutolewa kwa MKOPO

RASMI, Simba SC imesema itamtoa kwa mkopo kipa wake, Peter Manyika kwenda timu ambayo atapata nafasi ya kucheza kama chaguo la kwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema leo kwamba, Manyika bado ana miaka miwili ya kuendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo kulingana na mkataba wake, lakini msimu ujao atacheza timu nyingine.

Lengo la Simba ni kuokoa kipaji cha kipa huyo, mtoto kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Manyika Peter aliyewika Yanga SC. Hata hivyo, Hans Poppe hajasema Manyika anakwenda timu gani

Pamoja na Manyika, Simba imeachana na kipa wake mwingine mdogo, Dennis Richard iliyempandisha kutoka timu B.

Na Simba inaachana na makipa wake hao, baada ya kuwasajili kwa mpigo makipa namba moja na namba mbili wa timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula kutoka Azam FC na Said Mohammed kutoka Simba SC.

Manyika aliyesajiliwa Simba SC Julai mwaka 2014, amedaka jumla ya mechi 51 za mashindano tofauti, nyingi za kirafiki akifanikiwa kusimama langoni mara 30 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa huku akiwa amefungwa jumla ya mabao 34

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya