Simulizi:SEHEMU YA PILI: SIKUJUA KAMA YANGEKUWA HAYA Na GODFREY MPAGIKE

SIMULIZI; SIKUJUA KAMA YANGEKUWA             
                   HAYA.
SEHEMU YA PILI
Na GODFREY MPAGIKE.


ILIPOISHIA; Sitokaa niisahau siku ile ,,,,,,,,,,,,,,,,,,




Sitokaa niisahau siku ile ambayo kwa mara ya kwanza nilianza kuona kuku mgeni akiwa anaelekea kukata kamba, kulingana na matendo yake J nilihisi labda tayari kashaonja na katamani kuendelea na alichoonjeshwa.

Kama kawaida yetu mida ya jioni hatukuwa nyuma nasi katika muda wa ziada wa kujisomea usiku yani wazungu wanasema (preparation time), sikutaka kuamini yaliyokuwa yakitokea mbele yangu mpaka nilihisi labda ni ndoto kwangu kwa mambo ambayo JULIETH alikuwa akinifanyia kwani yalikuwa mageni kwangu kiasi cha kujiuliza mwenzangu kajifunzia wapi.
Ilikuwa ni muda wa kutoka mida ya saa nne usiku ambapo hakuruhusiwa mtu kubakia darasani, kwahiyo wale wa mabwenini walikwenda kulala na wale wa mtaani pia tulikuwa tukiondoka na kurudi majumbani kwetu. Tulitembea hatua kadhaa kutoka darasani kwetu na kwakua nyumbani kwetu hakukua mbali sana hivyo ilimpasa anidake mkono wangu mapema kabla sijatoka na kukaribia nyumbani.
Baada ya kunishika mkono wangu na viganja vyetu vikakutana pamoja na kutengeneza konde la pamoja ambalo lilikuwa lina siri kubwa ndani yake na bashasha za kutosha. Kwakua na mimi sasa nilikuwa najua nini labda kingeweza kutokea kulingana na hali iliyokuwepo kwa wakati huo.
Katika hali isiyo ya kawaida J akaniita kwa sauti nyembamba kama ya mtu aliyekuwa anaelekea kuomba hela ya kununulia nguo ya ndani kwa baba ake ambae kuonana kila siku anaingia usiku na kuondoka saa 11 asubuhi bila ya kuonana na watoto wake. Basi tukaendelea kusogea mbele na mwishowe tukasimama kabisa kwani J alikuwa anashindwa kuongea kabisa kwani alijawa na aibu huku akiendelea kutafuna kucha zake mpaka nikamwone huruma lakini nikaendelea kusubiri labda ni lipi analotaka kuniambia siku ile.

Basi kikapita kimya cha muda kama wa dakika tano hivi ndipo nikaamua kumwambia nahisi baridi na nataka kwenda kulala kwani ilikuwa tayari saa sita kasoro na bado hajaongea lolote. Nilipotaka tu kuondoka akanidaka mkono mwingine na kuning'ang'ania na kujihakikishia siwezi kuondoka na kumwacha kabla ya kuonge la kwake la moyoni.
basi hapo ndipo alipo jisogeza karibu kabisa na kifua changu na kisha baada ya muda mfupi akawa amegusa kabisa kifua changu huku akiendelea kunifukizia hewa yake iliyokuwa ikitoka kinywani mwake ikiwa na joto kiasi fulani kitu kilichonifanya nianze kusahau kuwa nilikuwa nahitaji kwenda kulala, basi hapo na yeye ndipo alijisikia vizuri zaidi baada ya kuona kama vile mawazo yangu yamebadilika zaidi,
wakati wa kutoa ya moyoni ulikuwa umekaribia, kwani kwa mara ya kwanza nilijikuta namuita baby neno ambalo sikutarajia kulitamka kwa siku ile, "Hapo ndpo na yeye akapata ujasili zaidi na kuniambia baby.....................ITAENDELEA KESHO MUDA KAMA HUU.


Usikose kufuatilia simulizi hii kila siku na audio zake pia ambazo zinamaliziwa muda si mrefu zitakuwa hewani.


USIWE MCHOYO WA SHARE KWA WENZIO PIA WAFURAHIKE
Imiendaliwa na GODFREY MPSGIKE
@Super Skeleton boy.
0759665229,0675748658.


Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya