Umemsikia sifa alizopewa MSUVA?
Kiungo wa timu ya mabingwa ligi kuu Tanzania Bara na Taifa Stars Simon Msuva.
Kiungo wa timu ya mabingwa ligi kuu Tanzania Bara na Taifa Stars Simon Msuva amepewa sifa na Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda, Mashami Vincent kuwa ni mmoja ya wachezaji wanaofanya vizuri na kumtabiria kufika mbali.
Vicent alitoa salamu hizo muda mchache kumalizika kwa mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya African Nations Championship (CHAN) 2017 ambapo ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kati ya Taifa Stars dhidi ya Amavubi ya Rwanda mchezo uliopigwa leo CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
"Msuva ni moja ya wachezaji wazuri ninaowafahamu kutoka Tanzania kwa muda mrefu naamini kwa kiwango chake atafika mbali kama ataendeleza juhudi zake za kucheza mpira kama hivi", amesema Vicent.
Kwa upande mwingine, Msuva ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ambao kwa muda mrefu amekuwa akiaminiwa na makocha wa timu ya taifa pamoja na klabu yake ya Yanga
Comments
Post a Comment