Kubemenda Mtoto
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa. Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi. Je, kuna ukweli wowote? Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa! kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi. Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi? unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kuj...
Comments
Post a Comment