AZAM FC WAWABURUZA VILIVYO WANA WA PALUHENGO


AZAM FC imeshinda mechi ya kwanza ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika ziara yake ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kuwachapa 4-0 wenyeji, Lipuli ya Iringa jioni ya leo Uwanja wa Samora, Iringa. 

Baada ya sare ya 0-0 na Mbeya City katika mchezo wa kwanza mjini Mbeya na kipigo cha 2-0 kutoka kwa Mji Njombe FC mjini Makambako, leo Azam FC iliamua kufanya kweli kujenga heshima. 

Dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hiyo ya kocha Mromania, Aristica Cioaba anayeingia katika msimu wake wa pili Azam FC ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0. 

Beki wa kati, Yakubu Mohammed ndiye aliyefungua biashara nzuri hii leo baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 26 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona ya Mghana mwenzake, winga Enock Atta Agyei. 

Dakika 10 baadaye, mshambuliaji mpya, Waziri Junior aliyesajiliwa kutoka Toto Africans ya Mwanza iliyoshuka Daraja, aliifungia Azam FC la pili. 

Kipindi cha pili pamoja na Lipuli inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa Simba, Suleiman Matola kukianza kwa kasi, lakini haikuchukua muda wakatulia na kuwaacha Azam kuendelea kutamba.

Kinda Yahya Zayid akaifungia Azam FC bao la tatu dakika ya 50, kabla ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kukamilisha shangwe za mabao kwa kufunga la nne dakika ya 60 
Kikosi cha Lipuli kilikuwa; Noel Etoga, Severine Chale, Emmanuel Kichiba, Ally Sonso, Martin Kuzila, Juma Nade, Salum Machaku, Goodluck Mwingira, Waziri Ramadhani, Jerome Lambele na Shaaban Ada. 

Azam FC; Mwadini Ali, David Mwantika, Bruce Kangwa/Abdul Omary dk87, Aggrey Morris, Yakub Mohammed, Frank Domayo/ Masoud Abdallah dk79, Bryson Raphael, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhan Mohammed dk86, Yahya Mohammed, Waziri Junior/ Joseph Kimwaga dk72 na Enock Atta Agyei/Idd Kipagwile dk69.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya