MSUVA ABAKIA ASHINDWA KENDA RWANDA


Image result for MSUVA
Mshambuliaji wa pembeni wa Yanga, Simon Msuva ameshindwa kwenda Rwanda.

Msuva ameshindwa kuungana na kikosi cha Taifa Stars kilichopaa kwenda Rwanda na amebaki Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza, Msuva alirejea Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizia mkakati wa uhamisho kwenda Morocco anakotarajiwa kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida.

“Ilikuwa aungane na wenzake wakiwa Dar es Salaam njiani kwenda Rwanda lakini imeshindikana,” kilieleza chanzo.

Hivyo Msuva yuko Dar es Salaam nafikiri atakuwa anaendelea na mipango yake.

Taarifa nyingine zinasema Msuva alifika hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) lakini hakufanikiwa kusafiri.

"Hatutajua kwa nini alishindwa, mwisho amerejea nyumbani kwake," kilieleza chanzo, jan

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya