YANGA YAANZA PROGRAM MPYA
Kikosi cha Yanga sasa kinahama kutoka Gym kwenda uwanjani.
Awali, chini ya Kocha George Lwandamina, Yanga walipasha misuli kwenye Uwanja wa Uhuru kabla ya kwenda kuanza mazoezi rasmi gym.
Lakini programu ya Lwandamina inaonyesha Yanga wanakwenda kuanza mazoezi uwanjani ikiwa ni kuanza rasmi kujenga mipango na mbinu.
“Ile ilikuwa ni kuimarisha miili yao, kinachofuatia sasa ni suala la kujenga kikosi na mbinu kwa ujumla,” kilieleza chanzo.
Comments
Post a Comment