PETER MSECHU, Akili kufumaniwa kila siku
Msanii Peter Msechu ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Yakawa' amefunguka na kusema mwili wake si tatizo kwani kila siku amekuwa akifumaniwa mtaani na watu akiwa na totozi za watu.
Msechu alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha 5 Selekt ambapo alidai licha ya kuwa na mwili mkubwa lakini mwili huo haumsumbui wala kumpa tatizo lolote kama baadhi ya watu wengine wanavyodhani na kusema amekuwa akiupigisha sana mazoezi ndiyo maana yuko fiti.
"Wakati Timbulo anasema mshumaa mambo ya kuachwa mimi na Yakawa yaani na wanawake wengi, mimi nafumaniwa kila siku kwa hiyo mimi na nguvu ya kujitahidi kwenda na mwili wangu huu, mimi nafanya sana mazoezi watu wengine ooh Msechu sijui mnene, mimi wanawake mtaani wanaongozana nasingiziwa kila kukicha watoto eti watoto wangu, kwa hiyo msinichukulie poa niko vizuri kila idara" alisema Msechu
Mbali na hilo Msechu anasema wimbo wake mpya na video yake imempa madeni makubwa kwani pesa zote amekwenda kufanyia video hiyo na kuwataka watu wasiishie tu kutumiana wimbo huo kwenye mitandao bali waangalie kwenye account zake 'You Tube' na kununua wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ambako ameuweka ila kumsaidia kupata fedha za kulipa madeni hayo.
Comments
Post a Comment