Kisa cha HAJI MANARA kuzaliwa familia ya YANGA lakini ni shabiki na msemaji wa SIMBA


                              Image result for HAJI MANARA
Kama ulikuwa hujui basi nakupa hii, afisa habari wa klabu ya Simba SC Haji Manara amezaliwa kwenye familia ya mchezaji wa Yanga, Sunday Manara ambaye ni baba mzazi wa Haji Manara alikuwa ni mchezaji wa Yanga na sasa amebaki kuwa mwanachama wa klabu hiyo.
Cha ajabu na kinachoshangaza ni kwamba, licha ya Haji Manara kuwa ni mtoto wa mchezaji wa Yanga bado yeye mapenzi yake yalikuwa pale mtaa wa Msimbazi kwa mnyama Simba na akakua akiwa anaipenda Simba.
Kutana na Sunday Manara baba mzazi wa Haji Manara kwasasa akiwa ni shabiki wa Yanga, mtoto wake Haji Manara ni mwanachama na msemaji wa klabu ya Simba, Sunday Manara amemuelezea mwanae kwa nini amekuwa shabiki wa Simba.
“Babu yake Haji mzaa mama alikuwa mwenyekiti wa Simba na tulikuwa karibu sana na yule mzee, haya ni mapenzi ya mchezo bado sisi wote ni wamoja tofauti za Yanga na Simba zibaki kwenye mapenzi ya mchezo wa mpira lakini iwe dhamira imejengeka na wote tunakusudia kujenga kitu kimoja, mpira wa Tanzania uende juu”, alisema Sunday Manara ambaye ni baba mzazi wa Haji Manara.
“Bahati mbaya fikra za watu wanafikiri Yanga na Simba ni uadui kwasababu hawaelewi, huu sio uadui. Mimi ninarafiki zangu wengi ni wapenzi wa Simba. Haji kwenda kwake Simba hakufanyi asiwe mwanangu, mimi ni mpenzi wa Yanga si mpenzi wa Simba”.
“Nina mwanangu mwingine jina lake Manara ni shabiki wa Simba, mtoto mdogo wa Haji ni shabiki wa Yanga, walishampeleka hadi klabu ya Simba wakampa soda na kilakitu wakamuuliza anapenda timu gani akasema Yanga lakini hakuna uhasama wala chuki”.

IMEKAAJE HII WADAU

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya