MANULA:Ndo basi tena simba

Kipa wa Azam, Aishi Manula.

WAKATI wachezaji wenzake wakitarajiwa kutambulishwa kwenye sherehe za Simba Day, kipa Aishi Manula atakosa fursa hiyo ndani ya kikosi cha Simba. 

Klabu ya Simba imekuwa na kawaida ya kuandaa tamasha mara moja kila mwaka ambapo huwa ni maalum kwa kukaribisha msimu husika ikiwemo kutambulisha wachezaji wao. 

Taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa kutoka kwa bosi mkubwa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na klabu yake ya Azam FC ni kuwa mkataba wa Manula unamalizika rasmi Agosti 10, mwaka huu huku dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa Agosti 6, mwaka huu. 

Imeelezwa kuwa kutokana na mkataba huo kumbana kipa huyo, itakuwa ngumu kwa Simba kukamilisha mchakato wa kumsajili bila kumalizana na Azam FC kwa kuwa ili asajiliwe lazima mkataba wake ndani ya Azam uvunjwe. 

“Mkataba wa Manula unatarajiwa kumalizika Agosti 10, mwaka huu, kwa maana hiyo kipa huyo hatakuwepo kwenye orodha ya wachezaji wapya watakaotambulishwa katika Simba Day. 

“Azam wanalijua hilo ndiyo maana unaona wapo kimya wanasubiri Simba wajichanganye, hizo taarifa kuwa mkataba unaisha Julai 30, mwaka huu siyo kweli lakini wanataka Simba wajichangaye ili wawageuzie kibao kwa kumsajili mchezaji ambaye bado yumo ndani ya mkataba,” alisema mtoa taarifa huyo. 

Hivi karibuni, Manula aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa mkataba wake na Azam unaotarajiwa kumalizika Julai 30, mwaka huu kitu ambacho kinapingana na uhalisia wa mkataba ulipo kwenye ofisi za TFF. 

Imekuwa ikielezwa kuwa Manula ameshasaini mkataba wa awali kujiunga na Simba kwa shilingi milioni 35, lakini ili Simba ifanikiwe kumtumia italazimika kuzungumza na Azam, kinyume na hapo ni kusubiri wakati wa dirisha dogo la Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu. 

Alipotafutwa Meneja wa Azam FC, Philip Alando alisema wachezaji wao waliokuwa Taifa Stars bado hawajajiunga na timu hiyo, lakini kuhusu Manula hana taarifa zake na wala hakutaka kuzungumzia suala la mkataba.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya