ANTONIO CONTE; MORATA ndiye chaguo langu la kwanza
Antonio Conte, amefurahia kukamilisha uhamisho wa straika wa Real Madrid, Alvaro Morata, na kueleza mara zote Mhispiania huyo alikuwa chaguo lao la kwanza.
Aidha, Conte amemtaka Morata kuthibitisha thamani yake na kusisitiza kuwa ndiye aliyekuwa chaguo lake la kwanza licha ya kwamba pia alimtaka Romelu Lukaku.
Conte alisema: “Huu ni usajili mzuri kwetu. Morata ni mchezaji kinda lakini ana uzoefu mkubwa na nyuma aliichezea Real Madrid na Juventus na ana uzoefu mkubwa kwenye ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bado ni mdogo na anaweza kujizatiti sana. Huu ni usajili mzuri kwetu.
“Kwa uhakika soko hili la usajili ni la kuchanganya, lakini si kwa msimu huu tu, ila sasa kuna fedha za kuchanganya. Kama unataka kununua mchezaji rahisi, mchezaji wa kawaida unayeanza kumfikiria utatumia Euro milioni 40-50.
“Hali hii ni ya kushangaza. Lakini kuna hali hii na lazima tuishi katika hilo. Ni sawa. Lukaku amegharimu kiasi kikubwa cha fedha, lakini ni sawa na Lacazette na Arsenal imetumia Euro milioni 65.
“Kwa beki mzuri unatumia Euro milioni 60-70. Hii ndiyo hali ilivyo sasa na lazima tuwe wazuri sana na kutofanya makosa wakati unanunua mchezaji. Lazima utumie kiasi kikubwa cha fedha na kuchagua ni muhimu sana.
“Morata ni chaguo letu la kwanza. Ni mshambuliaji mzuri, mchezaji mwenye matarajio sahihi kwa Chelsea. Anaweza kuonyesha thamani yake na sisi.
Comments
Post a Comment