KISA CHA MCHUNGAJI ALIYE MPA BIBLIA Simon Msuva
Mchungaji wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) la Rev Godlisten Nkya amempa zawadi ya biblia mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.
Msuva anatarajia kuondoka leo kwenda Morocco kujiunga na klabu yake mpya ya Difaa Al Jadid ambayo itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushika nafasi ya pili msimu uliopita.
Msuva ni muumini katika kanisa hilo, alikwenda kumuaga mchungaji Nkya.
Baada ya kusali pamoja, mchungaji huyo aliamua kumzawadia biblia.
Comments
Post a Comment