Simulizi( sehemu ya 1); SIKUJUA KAMA YANGEKUWA HAYA By GODFREY MPAGIKE

                                                                  NA GODFREY MPAGIKE.


UTANGULIZI
Karibu katika simulizi kali ya kusisimua itakayo weza kukusisimua ndugu msomaji na kuamsha hisia zako kwa yule umpendae. Hii inakuja kwako kama zawadi yangu kwakona ni hadithi yenye uhalisia ndani yake ambayo imewahi kunitokea ambayo inaweza kuwa na wewe imewahi kukutokea.

NIKWAMBIE; usikose kuifatilia simulizi hii kila siku saa mbili jioni (08:00) muda ambao utakuwa umepumzikabaada ya mizunguko mbalimbali ya maisha.


 SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa mwaka 1996 nilipopata kumfahamu JULIETH ambae ni tofauti kabisa na JULIETH wa sasa aliye jaa udar es salaam, mtoto wa kihehe aliyekuwa hajui kujivuna, mwenye staha mbele za watu asiyependa kujionesha mbele za watu labda niseme alikuwa ni kuku mwenye kamba mguuni aliyekuwa anasubiri mfugaji aamue kumchinja au kumuuachia aendelee kuishi akue.

Mwaka ule nilikuwa bado mdogo nisiyejua kuwa labda duniani watu hupendana na ndio wanaoweza kuja kukorofishana na kuonana maadui wakubwa wanaoweza kuja kupishana barabarani kama magogo yaliyosombwa na maji hayajui wapi yataishia huku yakigongana gongana, na kutojua labda yatajiokoa vipi.
Tulianza kujenga urafiki wetu polepole na kwakuwa na akili zetu fupi kama za kuku tukawa kama kama mtu na mdogo (maarufu ya shule za bweni, kuwa kaka mtu au dada mtu wa mtu usie mfahamu).Basi tuliendelea hivo hivo hadi miaka miwili ilipokata takamaliza elimu yetu ya msingi huku akilizetu zikizidi kukua siku hadi siku.
Baada ya hapo wote tulifanikiwa kufaulu wote na kuendelea na elimu ya sekondari mwaka 1999, hapo mimimnilifanikiwa kufanya mtihani mwingine kwaajili ya kujiunga na shule nyingine tofauti na ile niliyokuwa nimechaguliwa na serikali. Lakini mambo yangu yaligonga mwamba baada ya kukosa ada baada ya wazazi wangu wote kutoweka duniani, hivo ikanibidi nirudi palepale na maisha yaklaendelea tena kama kawaida.

Kwakua sasa hisia za mapenzi zilianza baada ya akili kukua na kujua nini mapenzi na labda yana nini ndani yake tukaanza kuoneana aibu na muda kidogo wa kukaa pamoja ukaanza kupungua. Vituko ndipo vikaanza vya kimapenzi siku hadi siku na kwangu nikaona kuwa ni kawaida labda mwenzangu anataka tuishi new style ya maisha kama wanavyosema waswahili siku zinzenda na maisha yanaenda.

Ilikuwa katikati ya mwaka wa masomo siku ambayo sitakaa niisahau pale JULIETH aliponitaka.........................itaendelea



by: Godfrey mpagike
@super skeleton boy.



                                                                 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya