Aishi Manula RASMI SIMBA
Golikipa Aishi Munula ambaye alikuwa anakipiga na klabu ya Azam FC amejiunga rasmi na klabu ya Simba na kesho atakwea pipa kujiunga na klabu hiyo ambayo sasa ipo nchini Afrika Kusini kwa maandalizi za msimu ujao. Kwa mujibu wa Haji Manara amesema kuwa klabu ya Simba imeshamalizana na mchezaji huyo na kudai ameahidi makubwa kwa mashabiki wa Msimbazi "Golikipa wa kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe moja, anatarajiwa kujiunga rasmi na kambi ya klabu yetu ya Simba iliopo Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini. Manula ambaye ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na klabu yetu, na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wetu, sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu" alisema Haji Manara Mbali na hilo Simba kesho inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini.