Ronald ashindwa kuokoa Jahazi



Chile imetinga fainali ya Kombe la Mabara kwa ushindi wa mabao 3-0, yote kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 za 0-0.

Kipa Bravo ambaye pia anadakia Man City, ndiye ameibuka shujaa baada ya kupangua penalti tatu huku Ronaldo akiwa anasubiri kupiga yake "baadaye".

Mchezo ulikuwa mgumu sana kama ulivyotarajiwa kati ya mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Chile ambao ni mabingwa wa America.

Mchezo huo wa nusu fainali ya confedaration cup ulimalizika dakika 90 kukiwa hakuna timu iliyopata bao na hata zilipoongezwa 30 ili kumalizia 120 milango bado ilikuwa ni migumu.

Baada ya hapo muamuzi aliamuru kupigwe mikwaju ya penati ambapo ndio Ureno waliondolewa baada ya Chile kufunga mikwaju yote mitatu ya mwanzo ya penati huku Wareno wakikosa.

Shukrani kwa mlinda lango wa Chile Claudio Bravo ambaye aliokoa penati tatu za Ricardo Quaresma, Moutinho na Nanj huku za Chile zikiwekwa kambani na Vidal,Sanchez na Aranguiz.

Baada ya mchezo huo ambao Bravo anyeidaki Man City alikuwa mchezaji bora wa mechi sasa Chile wanakwenda fainali wakisubiri mshindi kati ya Ujerumani na Mexico kwa ajili ya fainali hiyo ya Confedaration Cup.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya