Habari njema kipindupindu chapungua YEMEN

Habari njema! Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema katika juma lililopita idadi ya visa vya kipindupindu nchini Yemen, taifa linalokabiliwa na machafuko imepungua, hata hivyo shirika hilo limeonya kwamba katika msimu wa sikukuu ya Eid al-Fitr watu wengi nchini humo husafiri hatua inayoweza kuongeza maambukizi. 

Zaidi ya watu 200,000 wameambukizwa ugonjwa huo, zaidi ya 1000 wakifariki dunia tangu kuzuka kwa kasi mwezi Aprili mwaka huu. 

WHO imesema kwamba kusafiri kwa wakazi hao kusherehekea sikukuu hiyo kubwa nchini humo, kutawazuia wengi kutoenda hospitali, na kuongeza kuwa hilo litazingatiwa kwa tahadhari.. 
Dk Ahmed Zouiten ni mshauri mkuu wa dharura wa WHO 

''Tunatumaini kusema na kushuhudia kupungua kwa kiwango kikubwa, kwasababu ya juhudi zilizochukuliwa na WHO, UNICEF, na wadau wetu wengine katika sekta ya afya.''

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya