Tanzania VS Mauritius

Timu ya mpira wa miguu Tanzania, Taifa Stars inalizimika kupapambana kadri ya uwezo wao leo ili kushinda na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Angola mchezo uliyochezwa Jumapili iliyopita. 

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, inashuka dimbani leo kutupa karata yake nyingine dhidi ya Mauritius katika michuano ya kombe la COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. 

Stars imekuwa na maendeleo mazuri katika kikosi chake jambo ambalo limesaidia kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wake wa kwanza na kuweza kuleta matumaini makubwa kwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini. 

Mpaka sasa Stars wanaongoza katika kundi lake kwa pointi nne zenye magoli mawili huku wakifuatiwa na  Angola wenye goli moja na Mauritius na Malawi  wakiendelea kufurukuta

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya