Hatima ya MNYATE mikononi mwa SIMBA
Winga mwenye kasi Jamal Mnyate aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba msimu uliopita amefunguka na kusema kuwa bado ataendelea kuwemo katika klabu hiyo kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mwadui kwa mkataba wa miaka miwili lakini tangu alivyosajiliwa alifanikiwa kucheza mechi kadhaa kutokana na mara nyingi akiwa anasumbuliwa na majeruhi.
Amesema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kutokana na kuwa bado yupo chini ya mkataba na timu hiyo, lakini angekuwa ameshamaliza nao mkataba angekuwa huru kusema msimu ujao atakuwa wapi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu kusema msimu ujao nitakuwa wapi, kwasababu bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Simba kikubwa mimi nawasikiliza wao waajiri wangu watakavyonambia kuhusu hatima yangu,”amesema.

Comments
Post a Comment