Google yapigwa faini
Google imepigwa faini ya ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kuamua kuwa Google ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.
Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.
Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi.
Margrethe Vestager alisema kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU
Kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.
Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.
"Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU," alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU.
Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya Google tangu mwaka 2010
Uchunguzi huo ulianza kufuatia malalamiko kutoka makampuni kama Microsoft miongoni mwa mengine.
Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.
Comments
Post a Comment