Jay Zee afanya kufuru
PESA INAONGEA BWANA! Huku Beyonce akiwa amejifungua salama na kukaa hospitalini kwa muda wa wiki moja na nusu, hatimaye mwanamama huyo na watoto wake mapacha, wa kiume na kike wameruhusiwa kutoka hospitalini.
Habari zaidi kutoka katika ardhi ya US inatutonya kwamba baada ya watatu gao kuruhusiwa kutoka hospitalini, mumewe, Jay Z alikwishaandaa mjengo wa kupanga wa maana uliopo Malibu ambapo watatakiwa kulipia dola 400,000 (zaidi ya milioni 900) kwa mwezi tu.
Mjengo huo wa maana upo karibu na Bahari ya Pasifiki ambapo watapata muda wa kuangalia meli na watu wakila bata lakini pia mjengo una uwanja mdogo wa ndege. Mjengo una hekari 6.3, si hiyo tu, bado mtu mzima Jay Z anaendelea kusaka mjengo mwingine wa kununua huko L.A (Los Angeles)
Comments
Post a Comment