Mastaa waliohudhuria Harusi ya MESSI


Mastaa waliohudhuria kwenye harusi ya Messi, Argentina

 WACHEZAJI wenzake wa sasa na wa zamani Lionel Messi katika timu ya Barcelona wamewasili Argentina kwa ajili ya harusi ya mwenzao huyo anayemuoa Antonella Roccuzzo kesho.

Sergio Busquets, Jordi Alba, Carles Puyol, Cesc Fabregas, Xavi na Samuel Eto'o wote wameonekan katika picha iliyopostiwa kwenye ukurasa wa Instagram na mke wa Puyol, Vanessa Lorenzo.

Messi amewakaribisha wenzake wote katika kikosi cha Barcelona kwenye sherehe hiyo mjini Rosario, ambako wageni wamekodiwa hoteli ya nyota tano.

Mke wa Sergio Aguero, Karina ataimba wimbo wa kwanza katika sherehe hiyo.

Messi pia ameagiza kipikwe chakula cha kiasili cha 'locro' na 'empanada' ambacho ni nyama rosti kabisa ya Kiargentina pamoja na 'maanjumati' mengine.

Messi na mpenzi wake wa tangu utotoni hatimaye wataoana baada ya kukutana tangu wana umri wa miaka mitano mjini Rosario, Argentina walipokulia na wakaendelea kuwa pamoja hata mwanasoka huyo baada ya kuhamia Hispania alipofikisha umri wa miaka 13 kwenda kujiendeleza kisokaa. Na sasa wamerejea nyumbani kwao kabisa kwa sherehe hiyo kubwa kesho.

Messi na Roccuzzo, ambao wana watoto wawili, Thiago na Mateo, watafunga ndoa yao katikati ya mji wa Rosario, Santa Fe.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya