Faiza Ally amchana makavu Hamisa Mobeto

MSANII wa sinema Bongo, Faiza Ally amemchokonoa Video Queen, Hamisa Mobeto baada ya kunasa kibendi na kusema kuwa, anamshangaa mwanadada huyo kwa kutochagua mtu stahiki wa kuzaa naye. 

Akipiga stori na 3 Tamu, Faiza alisema kuwa, wasanii wengi hawajithamini miili yao na mfano mzuri ni mwanadada huyo ambaye anasikia ana ujauzito unaodaiwa ni wa msanii wa Bongo Fleva ambaye tayari ana familia yake na kuona alichofanya si sahihi. 

“Unajua wasichana wengi hawajithamini wanafanya vitu bila kufikiria, kama huyo Hamisa nasikia ana ujauzito wa huyo msanii (jina kapuni) na kama ni kweli mimba ni ya huyo mtu, kakosea sana, napenda kuongea kitu kinachonigusa kwenye nafsi yangu akichukia atajijua,” alisema Faiza. 

Msanii wa sinema Bongo, Faiza Ally

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya