MADONGO ya Manara kwa viongozi TFF

Baada ya taarifa za kukamatwa kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Celestine leo mapema msemaji mkuu wa klabu ya Simba (aliyesimamishwa), Haji Manara ametoa pole kwa viongozi hao.

Haji Manara amesema sisi kama wanadamu tunapitia changamoto nyingi sana hivyo ni bora tukafarajiana japo hata kwa kupeana pole pale mwenzio anavyopatwa na matatizo.

Haji Manara ambaye alipigwa ‘STOP’ na TFF ya kutokujihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja kwa makosa ya kinidhamu bado anaendelea na msimamo wake wa kuitumikia klabu yake ya Simba kama kawaida kwani alilitaka Shirikisho hilo limpe barua ya kumsimamisha.


Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya