Aliye kaa ardhini kwa siku 41 aibuka



MMOJA kati ya watu sita waliokaa siku 41 chini ya ardhi kufuatia kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Nyangalata, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Chacha Wambura, anaomba msaada wa matibabu. 


Wambura (51), alitembelewa na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake na kuomba msaada wa Sh. milioni 25 kwa ajili ya matibabu nchini India, baada ya matibabu yake kushindikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na gazeti hili mtoto wa Wambura, Marwa Chacha, alisema hali ya maisha nyumbani inazidi kuwa ngumu, licha ya kuishi maisha ya kimaskini na familia yao wako watoto 10 na wameishauza  ng’ombe 15 waliokuwa nao. 

Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikotibiwa Wambura kwa miezi sita, ubongo wake upande wa kushoto umesinyaa na kusababisha mwili mzima kutetemeka, hali inayomfanya kuzungumza kwa taabu. 

Wambura alifukiwa ndani ya machimbo ya Nyangalata, Oktoba 5 mwaka 2015, akiwa na wenzake Msafiri Gerald, Joseph Bulule na Amos Kuhangwa. 

Mchimbaji Onyiwa Kahindo alifariki dunia akiwa hospitali na Musa Supana alifia shimoni baada ya kukataa kula mende, vyura na magome ya miti na nguo walizokuwa wamevaa. 

Wambura aliomba mtu yeyote atakayeguswa anaweza kumchangia kupitia simu namba 0758 885 378 au 0757 650 301

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya