RATIBA Bundesliga yatolewa

Ujerumani. Mabingwa wa Bundesliga msimu wa 2016/17, Bayern Munich wamepagwa kuanza na Bayer Leverkusen mechi itakayochezwa Agosti 18. 

Bayen Munich ilitwaa taji la ubingwa ikiwa mbele pointi 15 msimu ulioisha, huku ikipoteza mechi mbili pekee mechi 34 za mashindano yote ya ligi hiyo. 

Mechi hiyo itapigwa kwenye dimba la Allianz Arena. Bayern Munich wataanza  kazi ya kutetea taji la ubingwa wakiwakaribisha timu hiyo iliyomaliza nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Bundesliga msimu uliopita. 

Shirikisho la Soka Ujerumani limetangaza ratiba hiyo ya msimu wa 2017/18 leo Alhamisi ambapo Borussia Dortmund watawafuata Wolfsburg ambao walinusulika kushuka daraja msimu uliopita. 

RB Leipzig waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Schalke ugenini huku wakitakiwa kujipanga vyema kwa ili kubakikwenye kiwango walichoonyesha msimu ulioisha

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya