MZEE Yusuf kufunga ndoa nyingine
Zikiwa zimepita siku kumi tangu apate pigo la kufiwa na mkewe mdogo, Chiku Khamis, aliyekuwa Mfalme wa Taarab Bongo na Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern, Alhaj Mzee Yusuf kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu endapo ataoa mke mwingine.
Mzee Yusuf amefunguka alipoulizwa na Gazeti la Risasi endapo hali yake itarejea kama kawaida, Mzee Yusuf alisema kuwa suala hilo ni la Allah, hivyo akiamua aoe ataoa na kama ameamua kumpunguzia ili atulie, basi atatulia.
“Suala la kuoa tena ni la Allah, nitamuomba kama akiamua mimi nioe nitaoa, kama pengine amenipunguzia ili nitulie basi nitatulia maana hili jambo linatakiwa subira kwa kila kitu, hutakiwi kukurupuka, nikikurupuka nitajikuta nashindwa mtihani huu ambao Allah amenipa,” alisema Mzee Yusuf.
Mke wa Mzee Yusuf, Chiku alifariki Juni 17, mwaka huu katika Hospitali ya Amana alipokuwa akijifungua na kichanga chake na kuzikwa katika Makaburi ya Kisutu, Juni 18, akiwa ameacha watoto wawili wa kike
Comments
Post a Comment