NAY WA MITEGO: Killer na Da prince wanashuka kwa kukosa radha


Nay Wa Mitego a.k.a True Boy, amedai kinachowatesa wasanii wenzake Young Killer na Barakah The Prince ni kwa kutokumbuka fadhila za watu waliofanikisha safari yao hadi kufikia walipo sasa. 

Naye wa Mitego amesema kuwa kinachowashusha na kuwasumbua wananmziki hao sio kuwa hawajui muziki isipokuwa hawana radhi za watu waliowanyanyua. 

“Young Killer hali yake ni mbaya, siyo yule ambaye tumemzoea, kashuka kabisa kimuziki na kwa alipofikia sasa tutegemee kuona akirudi Mwanza kuvua samaki, ila kama anataka mafanikio, basi arudi kuomba radhi kwa Monagangstar, producer ambaye alipoteza nguvu zake nyingi kumuonyesha njia kwenye muziki, lakini alipopata jina tu akamtema kwa jeuri. 

Kid Bway ndiye mtu pekee aliyepoteza muda wake na kumuhangaikia Baraka The Prince hadi akafika alipo sasa, lakini Baraka aliachana naye kwa maneno maneno mengi sana, ni kama laana inamtesa, anachotakiwa kufanya ni kwenda kumuomba msamaha ili aweze kukunjua nafsi, bila hivyo hawa watu wawili hata waimbe na Yesu hawatafanikiwa,” alisema Nay wa Mitego ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Elibarik 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya