MAUAJI YA WAWILI KIBITI
Mauaji mengine Kibiti! Usiku wa kuamkia leo Afisa Mtendaji kijiji cha Mangwi Kata ya Mchukwi na Mwenyekiti wake wameuawa kwa risasi na baadaye kuchoma moto nyumba.
My take:
Nasihi Serikali itazame jambo hili la MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji) kwa mtazamo mpana na wenye weledi. Tambo za IGP na Amiri Jeshi Mkuu zinaonekana ni maneno matupu. Wananchi wana haki ya kujua nini kinaendelea MKIRU.
========
Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).
Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.
Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa mauaji hayo.
Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.
Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwamo askari 13 wa polisi.
Chanzo: Mwananchi

Comments
Post a Comment