Jamali Malinzi hatoweza kushiriki uchaguzi TFF

Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais. 

Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo. 

Usaili wa viongozi wanaogombea uongozi TFF unafanyika kuanzia leo hadi keshokutwa wakati huo Malinzi atakuwa mahabusu. 

Malinzi amefikishwa leo mahakamani akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine. 

Baadhi ya mashitaka hayo ni kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa imeridhia kubadilishwa kwa Signatories (watu wanaosaini nyaraka za benki kutoa fedha). Shitaka hilo linawahusu Malinzi na Mwesigwa. 

Malinzi amedaiwa kugushi risiti za kwamba anaidai TFF na ziko risiti 20 ambazo anatuhumiwa kuzifoji. 

Shitaka jingine ni utakatishaji na hii wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Nsian wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha dola 375418

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya