SUMBAWANGA:Mwalimu ajiua aacha ujumbe mzito gest
Sumbawanga. Mwalimu, Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni mjini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema kwamba mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani.
Kyando amesema chanzo cha kifo cha mwalimu huyo bado hakijafahamika lakini aliacha ujumbe mfupi wa maneno.
“Kama anadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wake, lakini asilaumiwe chochote juu ya kifo chake," amesema Kamanda Kyando wakati akinukuu ujumbe huo wa marehemu.
Kamanda Kyando pia amesema uchunguzi wa kitabibu umebainisha kuwa mwalimu huyo alijiua kwa kunywa sumu
Comments
Post a Comment