Morrata akatisha fungate kukamilisha dili Man U

MSHAMBULIAJI Alvaro Morata amekatisha fungate lake Ibiza ili akashughulikie uhamisho wake kwenda Manchester United kwa mujibu wa gazeti la AS la Hispania. 

AS limeripoti kwamba Real Madrid amesafiri kutoka Ibiza kwenda nyumbani kwake mjini Madrid, huku mazungumzo ya uhamisho baina ya klabu hizo mbili yakiendelea. 

Morata amezungumza mara kadhaa kwa simu na kocha wa United, Jose Mourinho na imeripotiwa yuko njiani kuhamia Ligi Kuu ya England. 

Kocha wa United, Mourinho amekuwa shabiki wa Morata tangu anamfundisha katika kipindi chake cha kufanya kazi kwa miaka mitatu Bernabeu. 

Mashetani Wekundu 'walitupa ndoana' zao kwa Morata mwezi uliopita, lakini Madrid inataka ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 70 kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania. 

Mourinho anasaka mshambuliaji mpya Man United kwa sababu Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka siku si nyingi zijazo. 

Awali United walimtaka sana Antoine Griezmann, lakini Mfaransa huyo akaamua kusaini mkataba mpya Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kufungiwa kusajili. 

Mashetani hao Wekundu walimtaka pia mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku lakini bahati mbaya mchezaji hiyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameamua kurejea timu yake ya zamani, Chelsea. 

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya