Mahakama yamwachia huru Mpinzani wa NAPE


Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew na mwenzake Ismail Kupilila ambaye ni Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara.. 

Viongozi hawa walihukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017 na kufanikiwa kutoka kwa dhamana baada ya kukata rufaa na kukata hati ya ya dharura kwa ajili ya dhamana. 

Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Lameck Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili. Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia. 

Viongozi hao wa Chadema walihukumiwa kifungo cha gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana na kutoka kwa dhamana . 

Machi 7 mwaka huu Wakili wa viongozi hao wa Chadema, Deusdedit Kamalamo alisema kuwa baada ya mahakama kuwahukumu wateja wake kwenda jela miezi minane na kutoa nafasi ya kukata rufaa, walikata rufaa na kukata hati ya dharura kwa ajili ya dhamana. 

Mahakama Kuu iliwaachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Seleman Methew na Katibu wa Tawi wa kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila waliokuwa wakitumikia kifungo cha miezi minane kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali baada ya kuona kuna kesi ya kusikiliza. 

Kabla ya kutoa uamuzi wa kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2017, Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, alisikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na baadaye kuwaachia huru kwa kuwataka waweke dhamana ya sh. 2 milioni kwa kila mmoja. 

Viongozi hao wa Chadema wamekuwa gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya