TRUMP aanza vita na waislam
Rais wa Marekani, Donald Trump ameweka masharti mapya ya maombi ya hati za kusafiria kwa mataifa sita ya Kiislamu na wakimbizi duniani.
Moja ya masharti hayo ni kuwa anayeomba visa lazima awe na uhusiano na mtu mwenye ushirikiano wa kibiashara na Marekani.
Nchi zinazoguswa na masharti hayo ni pamoja na Iran, Libya, Somalia, Sudan Syria na Yemen.
Ujumbe kuhusu masharti hayo umetumwa katika balozi zote za nchi hizo.
Masharti hayo mapya yameanza kutekelezwa jana na yanagusa pia mahusiano ya kifamilia kama mzazi, mkeo ama mumeo, mtoto wa kiume ama wa kike aliye Marekani.
Masharti hayo yanatolewa baada ya Mahakama Kuu nchini Marekani kusitisha kwa muda agizo la Rais Trump la kuzuia nchi za Kiislamu kuingia Marekani, zuio ambalo lilikosolewa
Comments
Post a Comment