TETESI ZA USAJILI Ulaya leo
Kulikuwa na tetesi za chichini kwamba huenda Anthony Martial akaondoka United na kujiunga na Arsenal lakini leo Mfaransa huyo kutumia ukurasa wake wa Twitter aliandika “Les Remuers Sont Fausses” akimaanisha “tetesi zote ni uongo.”
Pierre Aubemayang inasemekana amepanga kuvitosa vilabu vya Ulaya vinavyomtaka na kusaini nchini China katika klabu ya Tianjin Quanjin ambayo inataka kumsajili Mgabon huyo kwa dau la euro mil 70.
Lakininpia taarifa zinasema mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata ambaye alikuwa visiwa vya Ibiza katika Honeymoon na mkewe ameamua kukatisha Honeymoon hiyo ili kurudi mjini Madrid kujaribu kufanikisha dili lake kuhamia Manchester United.
Wiki iliyopita tetesi zilisema klabu ya Juventus iko tayari kumuuza Alex Sandro kwenda Chelsea kutoka na ofa waliyotuma, lakini sasa dili hilo linaonekana kuwa gumu baada ya Manchester City nao kudaiwa kutuma ofa ya kumnunua Sandro.
Raisi wa Lyon Michel Aulas ameibuka na kudai kwa sasa Arsenal wasahau kuhusu Alexandre Lacazette kwani hakuna dalili ya kuondoka dirisha hili la usajili labda lijalo na akasema dirisha lijalo anaweza kuhamia katika ligi kuu ya Hispania.
Inasemekana klabu ya Manchester United hata ikimsajili Nemanja Matic bado itaendelea kuinasa sahihi ya kiungo wa Monaco Fabinho kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya kiung
Comments
Post a Comment