Bobi Wine aachiwa huru

Kampala. Mwanamuziki maarufu nchini Uganda, Bobi Wine ameachiwa leo, Jumanne muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi na kufikishwa katika Kituo Kikuu cha Kira. 

Bobi Wine alikamatwa mapema leo asubuhi kwa kukaidi amri ya kutofanya mkutano wa siasa katika eneo ambalo linakaribiana na mahali ambapo Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni alitarajia kuhutubia. 

Akizungumza muda mfupi baada ya kuachiwa, Bobi Wine amesema polisi wamemwachia baada ya mazungumzo mafupi na kwamba ataendelea na mkutano wake kama ilivyokuwa imepangwa lakini utafanyika eneo lingine. 

Bobi Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulanyi, ni mgombea binafsi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Kyadondo. 

Imeelezwa kuwa Bobi Wine alizuiwa kufanya mkutano leo katika eneo la Kasangati kwa sababu lipo kilomita chache kutoka eneo ambalo Rais Museveni alitarajia kufanya kampeni kumpigia debe mgombea ubunge wa chama chake cha NRM, Sitenda Sebalu.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).