Aliye kaa ardhini kwa siku 41 aibuka
MMOJA kati ya watu sita waliokaa siku 41 chini ya ardhi kufuatia kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Nyangalata, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Chacha Wambura, anaomba msaada wa matibabu. Wambura (51), alitembelewa na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake na kuomba msaada wa Sh. milioni 25 kwa ajili ya matibabu nchini India, baada ya matibabu yake kushindikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili mtoto wa Wambura, Marwa Chacha, alisema hali ya maisha nyumbani inazidi kuwa ngumu, licha ya kuishi maisha ya kimaskini na familia yao wako watoto 10 na wameishauza ng’ombe 15 waliokuwa nao. Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikotibiwa Wambura kwa miezi sita, ubongo wake upande wa kushoto umesinyaa na kusababisha mwili mzima kutetemeka, hali inayomfanya kuzungumza kwa taabu. Wambura alifukiwa ndani ya machimbo ya Nyangalata, Oktoba 5 mwaka 2015, akiwa na wenzake Msafiri Geral...