NGOMA NA KAMUSOKO KUONDOLEWA YANGA.


Wachezaji wazimbabwe THABANI KAMUSOKO na DONALD NGOMA,wameondolewa kwenye kikosi cha yanga kinachokwenda kuikabiri Mbeya city hapo kesho katika uwanja wa uhuru Dar es salaam.

HII ni kutokana na kutokuwepo kwenye mipango ya kocha mkuu wa timu hiyo yenye maskani yake jijini Dar es salaam,kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu

KAMUSOKO anayecheza nafasi ya kiungo na NGOMA anbaye ni straika, kwa sasa bado majeruhi na kocha LWANDAMILA amewatafutia mbadala wao ambao watacheza katika mechi hiyo.

Daktari wa Yanga Edward Bavu, amesema kuwa wachezaji hao bado wanamatatizo kwani KAMUSOKO anaumwa kifundo cha mguu na NGOMA anasumbuliwa na nyama za paja.
''KaMUSOKO na NGOMA wameondolewa kwenye mipango ya kocha kuelekea mchezo huo wa hapo kesho uwanja wa uhuru'' alosema Bavu

Kwa wiki zima wawili hao hawakufanya mazoezi ya maandalizi kuelekea mchezo huo wa hapo kesho na huenda wakaonekana mwezi ujao uwanjani kama watakuwa fiti.

Mara ya mwisho kwa nyota hao kuonekana uwanjani, ilikuwa ni mechi ya ligi kuu msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar, iliyopigwa septemba 30 kwenye uwanja wa uhuru ambapo mchezo ulimalizika kwa suluhu

CHANZO. CHAMPION

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya