“Wapiga Penati Wanaangalia Chini Kama Kondoo, Enzi zangu Bwana…”-Mwakyembe Atoa Somo Upigaji Penati


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa somo kwa wanasoka wa Tanzania kuhusu namna ya upigaji wa penati baada ya kutoridhishwa na namna ya baadhi ya wachezaji wanaopiga matuta nchini.

Waziri Mwakyembe amesema enzi zake alikuwa anawatungua magolikipa kwa mikwaju ya matuta tofauti na wapigaji wa siku hizi ambao huangalia chini mithili ya kondoo anaetaka kupigana.

“Upigaji penati nchi hii nafikiri nahitaji kukaa na makocha, sisi zamani tulikuwa tunafundishwa. Pale alikuwa hakosi penati, lakini vijana wa sikuhizi pamoja na ufundi mkubwa walionao, wanapiga penati wameangalia chini. Inashangaza mtu anaangaliaje chini? Wanabahatisha.”

“Mimi sipigi penati naangalia chini, najua toka niliposimama hadi kwenye mpira ni hatua sita, namwangalia golikipa movements zake, mguu wangu unaponyanyuka akianza kwenda kulia, mimi napiga kushoto, ndio upigaji wa penati. sasa mtu anaangalia chini utafikiri kondoo anakwenda kupigana.”

“Mimi ni mchezaji wa soka wa muda mrefu hata hao unaowasikia Tukuyu Stars sisi ndio tulianzisha huko miaka ya nyuma imeenda polepole tukiwa vijana wadogo tunacheza mpira, nilikuwa napiga namba tisa (9) vizuri sana.”

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya