Rais Mugabe Amtunuku Shahada Mke wa Jenerali Aliyemzuia

Rais Mugabe Amtunuku Shahada Mke wa Jenerali Aliyemzuia

 

Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano.
Marry Chiwenga alipata shahada ya MBA kulingana na shirika la habari la Zimbabwe.
Awali Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.
Alihudhuria sherehe za kuhitimu kwa mahafala kwenye mji mkuu Harare.
Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo.
Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.
Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya